Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Ruto afanya mkutano na CEO wa TikTok

Ruto Tiktok Rais Ruto afanya mkutano na CEO wa TikTok

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya, William Ruto leo Alhamisi asubuhi Agosti 24, 2023 amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok na kukubaliana kwa pamoja jinsi ya kufanya usimamizi wa maudhui kwenye mtandao huo hii ni baada ya TikTok kulalamikiwa kukiuka maadili ya Wakenya.

Itakumbukwa hivi karibuni Bunge la Kenya lilipokea ombi la TikTok kupigwa marufuku nchini humo hii ni baada ya Wadau hao kusema jukwaa hilo linaongoza kwa uvunjaji wa kanuni ya faragha na kusambaza maudhui ya ngono.

Spika wa Bunge la Kenya, Moses Wetang’ula alisema ombi hilo liliwasilishwa na Mtu aitwaye Bob Ndolo akidai TikTok inakusanya taarifa muhimu kutoka kwa Watumiaji wake pamoja na kutumika lkuhamasisha vurugu, lugha chafu, kusambaza maudhui ya ngono na matamshi ya chuki.

Katika mkutano huo wa mtandaoni (Online Meeting) na Rais Ruto Alhamisi asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa TikTok, Shou Zi Chew alijitolea kuhakikisha kuwa maudhui yanadhibitiwa ili kupatana na viwango vya jamii.

Maendeleo haya mapya yanamaanisha kuwa maudhui yasiyofaa au yanayokera yataondolewa kwenye jukwaa. Wakati wa mkutano huo, Chew pia alikubali kuunda Ofisi ya Kenya ili kuratibu shughuli zake barani. Aliahidi kuajiri Wakenya zaidi kufanya kazi kwenye jukwaa.

Haya yanajiri wakati Mkenya mmoja alipowasilisha ombi kwa Bunge la kupiga marufuku jukwaa hilo, akitoa mfano wa utangazaji wake wa maudhui chafu na nyenzo zinazotukuza ghasia.

Baada ya ombi hilo kuwasilishwa, mjadala mkali ulizuka miongoni mwa wabunge, huku maoni yakigawanyika kati ya kupigwa marufuku moja kwa moja na kutekelezwa kwa udhibiti mkali zaidi wa maudhui.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live