Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Museveni ameamua kuokoa maisha ya staa wa Kundi la Good Lyfe

2366 Sequence 01.Still0461

Thu, 1 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Uganda Yoweri Museveni leo ameripotiwa na vyombo vya habari kuguswa na tukio la ajali aliyoipata msanii wa Uganda kutoka Kundi la Good Lyfe, Rais Museveni ameguswa na hali ya sasa ya kiafya ya Radio ambaye hayupo sawa kiafya toka apate ajali ya gari January 22 2018.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Baada ya Rais Museveni kupata taarifa za Radio kuhitaji msaada wa kifedha ili kuokoa maisha yake kwa kukamilisha matibabu yake na kurudi kwenye hali yake ya kawaida, Rais Museveni ameripotiwa kutoa milioni 30 ili kuhakikisha Radio anarudi katika hali yake ya kawaida.

Radio

Hali ya kiafya ya Radio sio nzuri na mashabiki wake nchini Uganda wamepanga kufanya misa ya kumuombea siku ya Jumapili ya February 4 2018, kama humfahamu Radio ni moja kati ya member wa kundi la Good Lyfe linaloundwa na Radio na Weasel ambaye ni mdogo wa Jose Chameleon.

Radio akiwa hospitali baada ya kupata ajali.

Radio na Weasel wamefanya nyimbo nyingi ambazo zimewahi pia kupata Air time katika TV  na Radio Stations za Tanzania, Don’t Cry ft Wizkid, Zuena na wimbo wa Where You Are waliokuwa wameshirikishwa na Blu 3 na huu uliwafanya wajulikane zaidi Tanzania kutokana na wimbo huo kufanya vizuri.

Kutoka kushoto ni Radio na Weasel

“Mke wangu hawezi kutafuta kiki ana mtoto maarufu kushinda wewe”-Mose Iyobo

Chanzo: millardayo.com