Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli atamani Harmonize kuwa mbunge Tandahimba

80302 Pic+hamonize

Wed, 16 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema angetamani Mwanamuziki wa Bongo fleva, Rajab Abdul maarufu Harmonize awe mbunge wa jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumanne Oktoba 15, 2019 wakati akifanya mkutano wa hadhara mjini Ruangwa mkoani Lindi ambapo Harmonize alitumbuiza.

Akitoa shukrani na pongezi kwa watu waliotoa burudani katika mkutano huo, Rais Magufuli alisema “Lakumalizia nawapongeza sana waimbaji hawa wakina baba, lakini nampongeza sana Harmonize (Rajab Abdul) sijui anatoka jimbo gani? amesema Rais Magufuli

“Anatoka jimbo gani huyu? Tandahimba? Mbunge wa kule ni nani? Amehoji Rais na kueleza

“Aaa ningetamani kweli Harmonize akagombee kule akawe mbunge wa Tandahimba” amesema

Harmonize amekuwa akipewa nafasi ya kutumbuiza katika mikutano mbalimbali ya hadhara anayofanya Rais Magufuli.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

kila anapopewa nafasi ya kuimba, Harmonize anaimba wimbo wa ‘Magufuli’ ambao unaelezea mafanikio ya miradi mbalimbali iliyofanywa na kiongozi huyo.

Rais Magufuli yuko Ruangwa Mkoani Lindi kwenye ziara ambapo ameongozana na mkewe Mama Janeth, Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa, mawaziri na  manaibu waziri na   viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Chanzo: mwananchi.co.tz