Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Magufuli ampigia simu Diamond akiwa jukwaani Kigoma, yeye amhakikishia ushindi 2020

90511 Dai+pic Rais Magufuli ampigia simu Diamond akiwa jukwaani Kigoma, yeye amhakikishia ushindi 2020

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Rais wa Tanzania, John Magufuli ameisimamisha shoo ya kuadhimisha miaka 10 ya muziki ya msanii wa nchi hiyo, Diamond Platnum, baada ya kumpigia simu msanii huyo akiwa jukwaani.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatano Januari 1, 2020  katika uwanja wa Lake Tanganyika ambapo shoo hiyo ilikuwa ikifanyika. 

Ilikuwa majira ya saa 7:54 usiku akiwa amemaliza kuimba wimbo wa Tetema na msanii Rayvany, ambapo simu hiyo ilipelekwa jukwaani na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole  akiongozana na meneja wake Babu Tale.

Baada ya kuipokea aliwatangazia mashabiki waliofika uwanjani hapo kwamba, “wanakigoma nimewaambia kitu si nimewaambia leo mna bahati sana, kwenye simu tuko na Rais  Mheshimiwa John Magufuli, piga shangweeee, mheshimiwa shikamooo.”

Baada ya hapo akaweka sauti kubwa ambayo ilikuwa ikisikika kwenye spika, na kumwambia nakutakiwa wewe heri ya mwaka mpya pamoja na wanakigoma wote, wakati huo mashabiki wakawa wanapiga kelele za babu! babu! babu!.”

Kutokana na hali hiyo Diamond aliwatuliza lakini bado hawakusikia na kuendelea kupiga kelele.

Rais amesema alitamani na yeye angekuwepo hapo lakini amemtuma Polepole na wengine waliokuja hapo.

Diamond alimjibu, “baba watu tunakupenda sana na tunakuhakikishia awamu inayokuja unapita kwa kishindo sana, tunapiga mia kwa mia, Magufuli oyeeee! CCM oyeee!.”

Hata alipotaka kumuaga kwa kuwa ulikuwa ni usiku bado Rais Magufuli aliendelea kuongea na kusema, “ninawahakikishia wanakigoma hiyo barabara kutoka Kigoma kwenda Nyakanazi yenye zaidi ya kilometa 300  lazima ikamilike kwa lami, lakini nawapongeza sana wanakigoma.”

Rais aliwaaga wakazi hao kwa kuimba wimbo wa kiha  na kurudia kumpongeza tena Diamond  kwa kuwaambia  Diamond wewe ni mwanaume piga kazi.

Chanzo: mwananchi.co.tz