Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Japan aimba nyimbo za Diamond, Harmonize

77431 Majapan+pic

Fri, 27 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Raia wa Japan anayeishi nchini Tanzania, Ryuta Okamoto ametoa burudani ya aina yake leo jioni Alhamisi Septemba 26, 2019 katika Tamasha la Jumuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest).

Akiwa na gitaa mkononi aliimba wimbo wa Kwangwaru ulioimbwa na wasanii, Harmonize na Diamond.

Wakati mamia ya wananchi walioshiriki tamasha hilo wakidhani amemaliza, aliimba nyimbo za Mbagala na Nataka Kulewa za Diamond na kumaliza na wimbo wa Magufuli wa Harmonize.

Muda wote wakati akiimba nyimbo hizo alikuwa akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Ryuta amesema ameishi nchini kwa mwaka mmoja na miezi mitano na amekuwa na mapenzi makubwa na Tanzania licha ya kuwa anaishi kijijini ambako hakuna umeme.

“Nakaa kijijini hakuna umeme, maji nachota ya kisima lakini kwa kuwa nafanya kazi za kijamii wala sioni tatizo naipenda sana Tanzania,” amesema.

Pia Soma

Advertisement
Ryuta kwa taaluma ni ofisa maendeleo  na anafanya kazi katika Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma kwa kujitolea kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (Jica).

Amekuwa akihudhuria maonyesho mbalimbali na gitaa akiimba nyimbo za mastaa hao bila kujua maana zake.

Alipofanya mahojiano na Mwananchi Julai, 2019 amesema alijifunza nyimbo hizo kupitia mtandao ya Youtube.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz