Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rado amng'ata sikio Mondi

Rado Diamond.jpeg Rado amng'ata sikio Mondi

Sun, 6 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Movie RADO ameonyesha kukerwa na kauli ya Baba levo ya kusema wasanii wa Bongo movie ni manyumbu unaweza ukawaita hata 300 ukawapa elfu 30 na wasiseme jambo lolote.

Baada ya kauli hiyo wasanii wa Bongo Movie wamekuja juu sana mmojawao akiwa ni Rado na kusema kuwa Baba levo amekosea sana kuongea kauli hiyo kama angekuwa anamsema mtu mmoja bora angemtaja tu ila sio kutaja tasnia nzima.

Rado ameongeza kuwa tasnia ya Bongo movie imejaa watu wengi sana wa heshima akimtolea mfano Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa pia ni muigizaji kupitia Royal Tour ambayo inajulikana dunia nzima.

Rado ameenda mbali sana akimuonya Diamond kuwa makini na watu anaowaajiri waheshimu brand ya media yake huku akidai kuwa kwa sabbau Baba levo amefanya kosa itakuwaje wasanii wa Bongo movie waende mahakamani jee media aliyotumia kuongea neno hilo itakuwa salama???

Rado ameongeza kuwa ili Baba levo awe salama lazima aombe msamaha juu ya kauli hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live