Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rachel yupo kikazi zaidi 2018 – Linah

930 Screen Shot 2018 01 02 At 10.12.09.png TZW

Tue, 2 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki, Linah Sanga amefunguka kwa kusema kuwa alikaa chini na mwanadada Rachel Kizunguzungu na kumueleza nini anatakiwa kufanya ili asiyumbe kama mwaka 2017.

Linah akiwa na rafiki yake Rachel

Muimbaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa, amedai baada ya kumuona rafiki yake Rachel amepotea kwenye muziki kwa muda mrefu, alimua kumtafuta mrembo huyo na kukaa naye chini katika hatua nzuri ya kumueka sawa.

“Rachel ni rafiki yangu mkubwa, toka tukiwa THT tulikuwa pamoja na tulifanya kazi kwa kushirikiana sema hivi karibuni mwenzangu amekutwa na misukosuko ya maisha kitu ambacho ni cha kawaida katika maisha ya binadamu,” Linah aliimbia Bongo5.

“Lakini tayari nimeshakaa naye na tumezungumza mambo mengi na tumeelewana mwaka 2018 kwa Rachel utakuwa wa tofauti kabisa,” aliongeza.

Wawili hao tayari wameshaingia studio kwaajili ya kuandaa wimbo wao wa pamoja.

Chanzo: bongo5.com