Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ROMA amchana Nikki Mbishi kujenga chuki kwa wasanii

Www Roma na Nikki Mbish

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Rapa Roma Mkatoliki amemwambia ukweli Nikki Mbishi kwamba apunguze chuki na makasiriko kwa wasanii wenzake kwani inamaliza kipaji chake kwenye muziki.

Submitted by Shaluwa Anta on Ijumaa , 6th Aug , 2021 Roma Mkatoliki kushoto, kulia Nikki Mbishi

Roma amefunguka hilo baada ya Nikki Mbishi kusema Roma Mkatoliki amepata ukubwa baada ya taarifa za tukio la kutekwa akiwa na msanii Moni Centrozone mwaka 2017.

Kupitia Instagram ya Roma ameandika kuwa "Nikki punguza chuki, chuki zinamaliza kipaji chako, fanya muziki acha makasiriko kwa wasanii wenzako, ccha chuki haikujengi inakubomoa kila leo"

"Kuna wakati unasingizia hiyo Life style yako au hiyo ndio HipHop, Big no! HipHop sio chuki, HipHop ni love & peace, utamaduni wa HipHop hautufundishi chuki, unatufundisha unit".

Chanzo: eatv.tv