Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makonda kujenga studio ya muziki Dar ‘Dar Music Hub’

5097 WhatsApp Image 2018 03 18 At 15.31.53.jpeg TZW

Tue, 20 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza neema kwa wasanii wa muzuki kwani amempata mdau ambaye amekubali kujenga studio ya kurekodia muziki ya mkoa wa Dar es salaam, Dar Music Hub.

RC Makonda



Akiongea na waandishi wa habari wiki hii, Makonda amesema lengo lake ni kuboresha mazingiza ya kufanyia kazi ya wasanii wa mkoa wa Dar es salaam.

“Wasanii wakitaka kwenda kurekodi nyimbo zao wanatoa pesa nyingi, na pesa hawana, na hawa ni wasanii ambao wanataka kufanya kazi kupitia vipaji ambavyo mwenyezi mungu amewapa,” alisema Makonda.

Aliongeza, “Nina habari njema kwa hawa ndugu zangu, nimepata mdau atakayetujengea studio ya mkoa Dar es salaam, Dar Music Hub ambapo wasanii wote watarekodi bure, na hatuta ishia hapo, tunaandaa utaratibu wa kuwakopesha wasanii. Kwa mfano Bongo Movie wanataka kushoot movie, wanaweza kuchukua pesa na wakarudisha kwa gharama nafuu,”

Pia Makonda wiki iliyopita alitoa ruhusa kwa wasanii ndani ya mkoa wa Dar es salaam kushoot video na movie zao katika maeneo yoyote bila kusumbuliwa na mamlaka.

Chanzo: bongo5.com