Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

R. Kelly ashambuliwa gerezani

R Kelly Attacked In Jail Cell 660x400 R. Kelly ashambuliwa gerezani

Sat, 29 Aug 2020 Chanzo: millardayo.com

Moja ya taarifa iliyopo kwatika Mtandao wa TMZ ni kumhusu Wakili wa R. Kelly ambapo ameomba mteja wake achiliwe huru mara moja baada ya kusemekana kwamba ameshambuliwa na mfungwa mwenzake.

Steve Greenberg amesema mteja wake alishambuliwa katika kituo cha kurekebisha tabia cha Chicago, ambapo Kelly anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake dhidi ya madai ya unyanyasaji wa kingono.

Kiwango cha majeraha bado hakijafahamika, Bwana Greenberg amesema kupitia mtandao wa Twitter.

Kelly hajapatikana na hatia kwa makosa kadhaa ikiwemo ya unyanyasaji dhidi ya watoto na biashara ya ngono.

Taarifa za madai ya kushambuliwa kwake kuliripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya habari ya TMZ, ambayo imesema kwamba mfungwa mwenzake alianza kumpiga Kelly ngumi akiwa ameketi kwenye kitanda chake.

KIJANA ALIYEFARIKI TUNDUMA KATIKA VURUGU AZIKWA, “TUNAMLAZAJE MTOTO AMBAYE HATUWEZI KUMUANGALIA”-DC

Chanzo: millardayo.com