Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

R.Kelly apatikana na hatia ya kuwarekodi watoto video za ngono

R Kelly Denied Bail 660x400.jpeg R.Kelly apatikana na hatia ya kuwarekodi watoto video za ngono

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki kutoka Marekani, Robert Kelly maarufu R.Kelly amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono wa watoto katika kesi ya pili iliyoendeshwa namahakama ya shirikisho.

Jopo la mahakama lilimpata Kelly na hatia ya makosa sita kati ya 13 katika kesi ya wiki nne iliyoendeshwa katika mji wa anaomishi wa Chicago.

Mahakama ilimuondolea kesi ya jimbo ambayo ilipaswa kubaini iwapo kuna ushahidi kuhusu mashitaka ya ponografia ya watoto katika mwaka 2008.

Mwaka jana muimbaji huyo wa Bump n’ Grind alipatikana na hatia ya usafirishaji haramu wa watu kwa ajili ya ngono nakuhusika na njama za wizi na ulaghai mjiniNew York. Baadaye alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

R.Kelly ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, alipatikana Jumatano na hatia tatu za kuwalaghai watoto kwa ajili ya ngono na makosa matatu ya kutengeneza picha za ngono za watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live