Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Queen Darleen kurejea kwa kasi

3c69c213e542b3b0c98e5c219857c60d.jpeg Queen Darleen kurejea kwa kasi

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

NYOTA wa muziki kutoka lebo ya Wasafi, Mwanahawa Juma ‘Queen Darleen’ amesema amechelewa kurudi katika muziki kutokana na kusumbuliwa na ujauzito.

Msanii huyo alisema baada ya kupata ujauzito ulikuwa ukimsumbua na kupelekea kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, msanii huyo alisema baada ya kufanyiwa upasuaji ilibidi atulie muda mrefu ili aweze kupona kidonda cha upasuaji kisha arudi tena kwenye muziki.

“Kutokana na kujifungua kwa upasuaji nisingeweza kurudi kwa kasi katika muziki, nilihitaji kupumzika kwa muda mrefu hadi nipone na sasa naendelea vizuri na sasa nipo tayari kurejea kwa kasi,” alisema.

Oktoba, mwaka jana Darleen alijifungua mtoto wa kike aliyezaa na mume wake Isihaka na kumpa jina la Balqis.

Alisema kwa sasa mambo yanakwenda vizuri na muda sio mrefu atarejea tena akiwa na nguvu mpya na kasi hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kusubiri mambo mapya.

Darleen aliyeanza muziki miaka ya 2000 aliwahi kuvuma na ngoma zake mbalimbali kama Bachela, Nitakufilisi, Touch, Mbali, Wajua nakupenda na Kijuso.

Chanzo: habarileo.co.tz