Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Queen Darleen afunguka baada ya ndoa yake kuvunjika

Queen Darleen Queen Darleen afunguka baada ya ndoa yake kuvunjika

Fri, 30 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Queen Darleen; ni msanii wa Bongo Fleva aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ya Diamond Platnumz ambaye ameibuka kusema kwamba acha watu wamuone mjinga baada ya kuachana na ndoa.

Darleen ambaye alifunga ndoa na mfanyabiashara Isihaka Mtoro kabla ya mambo kwenda mrama anasema kuwa, baada ya kuchukua hamsini zake, kwa anaishi maisha yenye furaha kuliko wakati alipokuwa ameolewa.

Darleen amesema hayo wakati akitoa maoni yake kuhusu habari ya kusikitisha ya mwanamke wa Nigeria aliyefariki dunia wakati akikimbizana kwa gari na mume wake aliyekuwa na mchepuko ndani ya gari linguine.

Mwanamke aliyefariki alikuwa mwanasheria ambaye imeelezwa kuwa alikuwa anapitia manyanyaso ndani ya ndoa na pia mumewe husika alikuwa hajatulia, anaendekeza umalaya na kutoheshimu misingi ya ndoa.

Inadaiwa pia kwa sasa aliyekuwa mume wa Queen Darleen yupo na mwanamke mwingine ukiacha yule mke mkubwa, Sabra ambaye ilisemekana walimaliza tofauti zao za awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live