Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Queen Darleen: Nje ya ndoa naishi maisha ya furaha

Queen Darleen Ndoa Queen Darleen

Fri, 23 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Queen Darleen ameibuka kusema kwamba acha watu wamuone mjinga ila baada ya kuachana na ndoa na kuchukua njia yake kwasasa anaishi maisha yenye furaha kuliko wakati alipokuwa ameolewa.

Queen Darleen amesema hayo wakati akitoa maoni yake kuhusu habari ya kusikitisha ya mwanamke wa Nigeria aliyefariki dunia wakati akikimbizana kwa gari na mume wake aliyekuwa na mchepuko ndani ya gari jingine.

Mwanamke husika ambaye alikuwa mwanasheria imeelezwa alikuwa anapitia manyanyaso ndani ya ndoa na pia mume husika alikuwa hajatulia anaendekeza umalaya na kutoheshimu misingi ya ndoa.

Indaiwa pia kwasasa aliyekuwa mume wa Queen Darleen yupo na mwanamke mwingine ukiacha yule mke mkubwa ambaye walielezwa waliondoa tofauti zao za awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live