Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Queen Darleen: Nimepitia masahibu mazito

Queen Darleen Ndoa Darleen na mumewe

Sat, 23 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanahawa Abdul almaarufu Queen Darleen; ni mwanamama wa Bongo Fleva ambaye anasema amepitia masahibu mazito kabla ya kuamua kutoka kwenye ndoa yake na mfanyabiashara Isihaka Mtoto.

Darleen ambaye ni mama wa watoto wawili anasema kuwa, ni kweli hayuko kwenye ndoa kwa sababu ameona ni bora kupumzika maana aliyokutana nayo ni mazito.

Akizungumza, Darleen anasema kuwa, ameamua yote hayo kwa sababu anampenda mtoto wake na asingependa amuache mapema.

Darleen anasema kuwa, alikuwa anasikia uchungu, lakini ameacha kila kitu pembeni ili tu awe na amani ya moyo kwenye maisha yake.

“Najua watu wanaweza kunicheka sana. Ni kwa sababu tu hawajui ukweli wa masahibu mazito na ya kuumiza ambayo nimeyapitia kwenye maisha yangu na ndoa yangu.

“Cha kujua tu ni kwamba nipo singo tu, nimemwaga manyanga sasa kwa ajili ya mwanangu na simchukii baba mtoto wangu,” anasema Darleen ambaye amezaa mtoto mmoja na Isihaka aitwaye Balqis Isihaka.

Darleen aliolewa mke wa pili na Mtoro ambapo walijaaliwa mtoto mmoja, lakini ndoa yao haijawahi kuwa na utulivu wa hata mwaka mmoja kwa kile kilichodaiwa kuwepo kwa maelewano hafifu kati ya Darleen na mke mkubwa aitwaye Sabra.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live