Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Queen Darleen: Nampenda Isihacka kufa

Isihaka Na Darleen Queen Darleen: Nampenda Isihacka kufa

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Queen Darleen amesema licha ya kwamba kwa upande wake hayupo kwenye ndoa lakini anampenda sana mume wake, Isihacka.

Akizungumza na Wasafi TV, Queen amesema kuna vitu vilitokea ndani ya ndoa vinavyomfanya yeye atamke kuwa hayupo kwenye ndoa na kama Isihacka atamruhusu avizungumze basi atasema.

“Sipo kwenye ndoa lakini nampenda sana huyo mwanaume. Nimezaa naye hivyo hata nikisema nini bado ni mwanaume wangu, nina mtoto naye,” alisema Queen.

Mrembo huyo memba wa WCB amesema kwa sasa anachoamini kwa sasa kilichobaki ni kulea mtoto tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live