Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Kassim Ally maarufu kama Juma Nature amegoma hakutumbuiza kwenye Tamasha la Wasafi Festival mjini Mtwara Wikiendi iliyopita.
Baada ya Juma Nature kuweka wazi sababu za kutofika kufanya shoo ya Wasafi Festival Mtwara kisa walitaka kumlipa Tsh 500,000 jambo ambalo amechukulia kama dharau.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Q Chillah ameandika kuwa;
“We Baba Levo unaonyeshaga kadi zako za gari nyumba hebu tuthibitishie Watanzania kwa maaandishi juma au TNC wamechukua 10 kwanza au mlimpa Chege maana roho yake inafanana na Kigoma.”
Q Chillah ameongeza kuwa; “We mdogo wangu Baba Levo ukitaka tuzungumze utaweza kweli deal na juma kwanza mi nadeal ba kina boss zako we ongea na wasichana na machawa au mpaka myu afe ujichangishe pesa miingi na macamera toa sasa epuka lawama malizana tu na mtu tulia bana.”
Hii yote ni kutaokana kauli iliyosambaa mitandaoni siku ya jana baada ya Juma Nature kuulizwa nna shabiki mbona hakuonekana kwenye Tamasha la Wasafi Festival Mtwara licha ya kufanyiwa Promo kuwa atakuwepo?
Juma Nature alijibu kuwa hakufanikiwa kwenda kwa sababu hakuridhika na malipo ya show maana walitaka kumlipa laki tano tu.
Baada ya kauli hiyo ya Juma Nature, Baba levo ambaye ni mtangazaji wa Wasafi Media alisema kuwa kwenye Tamasha lao hakuna msanii anayelipwa chini ya milioni 10.
Unaadhani nani mkweli kati ya Juma Nature na Baba levo?