Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Q Chief atangaza kumaliza bifu na TID

Q  CHIEF Q Chief atangaza kumaliza bifu na TID

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Bongo Fleva, Q Chief ameweka wazi kuwa mwaka huu 2024 hataki tena kuwa na tofauti na mkongwe mwenzake TID.

Chilla ameandika kuwa wamekuwa mahasimu kwa muda mrefu bila faida yoyote hivyo haoni umuhimu wa kuendeleza tofauti zao.

Lakini pia Q chief amempongeza TID kwa harakati zake za kimuziki anazozifanya kwa sasa.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Chillah amesema; "Anaitwa Khalid Mohammed au Kigogo Warioba. Leo nachukua nafasi hii kuanza rasmi mwaka 2024 kwa staili ya kikubwa na tofauti.

"Nitaaanza kwa kukupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya katika harakati zako Nimevutiwa sana na jinsi inavyopambana unastahili pongezi. Lakini pia nichukue nafasi hii kukujuza kwamba, sina tofauti zozote kati yangu mimi na wewe.

"Ule ugomvi usio na maaana wala malengo umefikia tamati kuna kesho tusije shindwa kuja kuzikana kisa watu ama vitu vidogo.

"Hatua ni sehemu ya ukomavu na ujasiri katika maisha. Mwenyezi Mungu atupe mwisho mwema. Sijui lakini cant wait to see us on one stage. Nuff lv nuff respect @tidmusic @cloudstv, @mwanafa @majani. Ni yeyeeeeeeeeeeeee vujuvenga watoto wadogo," amesema Chillah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live