Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Q-Chief ampongeza Juma Nature kugomea shoo ya Wasafi Festival

Chief Nature Q-Chief ampongeza Juma Nature kugomea shoo ya Wasafi Festival

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Juma Kassim Ally maarufu kama Juma Nature amegoma hakutumbuiza kwenye Tamasha la Wasafi Festival mjini Mtwara Wikiendi iliyopita.

Baada ya Juma Nature kuweka wazi sababu za kutofika kufanya shoo ya Wasafi Festival Mtwara kisa walitaka kumlipa Tsh 500,000 jambo ambalo amechukulia kama dharau.

"My dearest brother moja kati ya wasanii pendwa mwenye records zako za kutosha and still you stand alone kwanza kabisa nikupongeze kwa msimamo wako juu ya hili itoshe kusema juma amefanya mengi na anastahili more respect sio huo ujinga.

"Mtu aliyekuletea mzigo wakutoshaa juzi tu leo ukamrubuni kwa Tsh 500,000 atafanyia nini zaidi yakulewea? Walah ni aibu kubwa kwa kampuni kubwa umejitambua thamani yako kubwa hujawahi kukosa riziki kila siku una-show hiyo ni karma na sio kila mtu anayo itunze, there still time.

"Ruge kafa na mengi sana kasemwa kasimangwa show zake zinaumiza anawatumia watu, ila tangu aondoke mpaka leo bei zilezile why? Juzi tu kakupa fuko la dollar tena za kutosha, kaondoka teee, its time to change our image.

"Misimamo sio ujeuri ni grows which to you sounds like lack of discipline, mlikuwa na muda wa kujitafakari na kuitafakari safari ya kaka yetu Nature, but you ignored, mdogo wangu kama utaendelea hivi na Tale kuna siku utasikitishwa believe, you have time to change, be real, stop acting," amesema Q-Chief.

Wasafi Festival ilizinduliwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara na baada ya hapo itasogea mpaka Dimba la Kassim Majaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live