Licha ya maisha binafsi ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin kugubikwa na usiri mkubwa, afisa huyo wa zamani wa KGB mwenye umri wa miaka 71 ameripotiwa kuhusishwa kimapenzi na mwanamke mrembo aliyesomea nchini Uingerza.
Mwanamke huyo anayekwangua moyo wa Putin si mwingine bali ni Ekaterina "Katya" Mizulina mwenye umri wa miaka 39 na Binti wa mfuasi mkubwa Putin, Seneta Elena Mizulina.
Katika siku za karibuni mwanamke huyo amepewa jina "Mlezi wa maadili wa Putin" kutokana na kazi anayoifanya mtandaoni ya kupingana na wakosoaji wa dikteta huyo, haswa kuhusu vita vya Ukraine.
Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Urusi Olga Romanova aliiambia Idhaa ya 24 ya Ukraine: "Katya Mizulina ndiye aina ya wanawake ambao Putin anawapenda".
Hata baadhi ya wananchi wa Urusi wanadai kwamba Ekaterina Mizulina ana muonekano ambao unamvutia sana Rais wao.