Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Pumzi ya Mwisho’ kutoka kwa Vanessa Mdee kunufaisha familia ya Mubaraka Mwishehe

1574 Screen Shot 2018 01 19 At 13.19.45.png TZW

Fri, 19 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki anayefanya vizuri kwa wanawake Bongo, Vanessa Mdee amebainisha ngoma ya ‘Pumzi ya Mwisho’ kuwa ni moja ya ngoma anayoikubali katika albamu yake ya Monday Money ambayo ina kionjo cha ngoma ya marehemu Mubaraka Mwishehe iitwayo ‘Jogoo la Shamba’

Vanessa amebaisha  kuwa kabla ya kutoa ngoma hiyo ya ‘Pumzi ya Mwisho’ aliyowashirikisha marapper wakali Joh Makini na Cassper Nyovest alifika nyumbani kwa marehemu Mubaraka Mwishehe na kuonana na familia yake ili aombe idhini ya kutumia kionja katika ngoma ya nguli huyo wa muziki wa dance pia kuona familia hiyo itanufaika vipi na mauzo ya ngoma hiyo.

“Pumzi ya mwisho ni wimbo ninao upenda sana kwenye ulbum yangu ya #MondayMondays. Ni moja kati ya nyimbo zangu bora kwenye album. Sababu kubwa ya Mimi kuchagua beat ya huu mwimbo ni kionjo kimoja kutoka kwenye wimbo wa hayati MBARAKA MWINSHEHE #Legend kabla ya album kutoka nikaona ni vema kuwaona familia ya MBARAKA kwanza ili nipate idhini ya kuendelea na kazi hiyo na kuona watanufaika vipi kama familia kupitika huo wimbo. Nashukuru walinipokea vizuri sana na walitoa idhini yao kwa mikono miwili kabisa.,” ameandika Vanessa katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Akaongeza “Nusu ya mauzo ya wimbo huu kwenye mitandao ya kidigitali yataenda kwenye familia ya Mzee Mwinshehe siku zote. Nisingeweza kukamilisha kazi hii bila mkono wa @s2kizzy producer, Sauti ya @CassperNvoyest kutoka #SouthAfricana Mwamba @johmakini asanteni sana. Kuna mengi tuliongea kuhusu mzee ya kusikitisha na kufurahisha pia unaweza kuona video yote ukiwa na #VeeMoneyApp inapatikana kwenye store zote #PlayStore na #AppStoreAsanteni sana #MoneyMondays#PumziYaMwisho.

Chanzo: bongo5.com