Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Programu inayoonyesha mfano wa sura mtu akizeeka yachangamkiwa

67270 Challedpic

Thu, 18 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Unaweza kusema programu ya FaceApp kwenye simu janja (smartphone) unayoweza kutumika kubadili picha ya mtu na kuonekana atakavyokuwa amezeeka, imeiteka mitandao ya kijamii.

Hali hiyo inatokana na watu wa kada mbalimbali kubadili picha zao na kuzisambaza mitandaoni jambo linaloibua mjadala miongoni mwa watu wanaofahamu mwonekano halisi wa mhusika.

Programu hiyo imezidi kuwa maarufu baada ya watu mashuhuri kuanza kuweka picha hizo wakiwemo wanamuziki wa Marekani, Kanye West, Drake na Ludacris,

FaceApp ilitengenezwa mwaka 2017 hadi sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 80 duniani kote.

Programu hiyo imefanyiwa marekebisho zaidi ya 20 na iliyopendwa zaidi ni ile inayoweza kuonyesha jinsi mhusika atakavyokuwa akizeeka.

Hata hivyo, baadhi ya watu wameipinga programu hiyo kutokana na madai kuwa moja ya masharti yaliyowekwa ni mtumiaji akiitumia picha yake aliyoifanyia maboresho itatumiwa na wasimamizi wa programu hiyo.

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz