Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Jay kurudi kwa kishindo

28596973725448570910f812aa527245.png Profesa Jay kurudi kwa kishindo

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa Bongo Fleva, Joseph Haule, ‘Profesa Jay’, amesema ana mipango wa kuachia kazi ili kuendelea kuwafurahisha mashabiki wake.

Profesa Jay alitoa kauli hiyo siku chache baada ya kushirikishwa kwenye wimbo wa ‘Baba‘ unaovuma akishirikishwa na msanii Boniventure Kabongo ‘Stamina’.

Kupitia kwenye mtandao wake wa Instagram, Profesa Jay aliwajulisha mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani mipango yake kwa sasa nikuachia kazi .

“Nadhani sasa umewadia muda muafaka wa kuachia nyimbo mpya, kuachia kazi baada ya kazi ili kuwafurahisha mashabiki wangu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,” alisema Profesa Jay

Profesa Jay ambaye alikuwa mbunge wa Mikumi alisema shughuli za kuwawakilisha wananchi zilikuwa zinamkosesha muda wa kutunga nyimbo hivyo anaamini kwa sasa ana muda wa kutosha kuendelea na tasnia hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz