Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Jay kuachia kazi mpya

C2e8ec7ff7fc61bb3f186b4739a548a4.png Profesa Jay kuachia kazi mpya

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule au Profesa Jay amesema anatarajia kuachia kazi mpya April 8, mwaka huu baada ya kumalizika siku 21 za maombolezo ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Profesa Jay awali alikuwa aachie kazi mpya kabla ya kifo cha Rais Magufuli ambaye siku chache kabla hajafariki alimsifia msanii huyo kwa wimbo mzuri wa Baba alioimba na Stamina kwamba una ujumbe mzuri kwa jamii.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Profesa Jay aliweka ujumbe kuhusu kazi hiyo mpya kuwajulisha mashabiki zake kwamba sasa anarudi mtaani baada ya kutoka kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Mikumi Morogoro kwa miaka mitano bungeni.

“Nawashukuru sana wote kwa ushauri wenu, sasa ni rasmi kuwa tutaachia lile jambo letu April 8, mwaka huu baada ya siku 21 za maombolezi kuisha, asanteni sana kwa ushirikiano mkubwa mnaoendelea kunipa,” alisema.

Nyota huyo licha ya kwamba alikuwa Mbunge kabla ya kukosa kipindi cha pili mwaka jana, alikuwa akipenda kazi hiyo ya sanaa na kuifanya kwa muda mrefu.

Profesa J ni miongoni mwa wasanii waliodumu kwenye sanaa kwa muda mrefu wakikubalika kutokana na kutoa kazi zenye ujumbe mbalimbali kwa jamii.

Alianza muziki miaka ya 90 akiwa na kundi la Hard Blasters na wimbo uliowahi kuvuma enzi hizo unafahamika kama Chemsha Bongo na tangu hapo amekuwa akitoa kazi mpya nyingi na kuimba na wasanii kibao.

Chanzo: www.habarileo.co.tz