Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Jay atoa  somo la ndoa

D457de4c68f3121dc6efcd98eef23b66 Profesa Jay atoa  somo la ndoa

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII mkongwe wa Bongo Fleva, Joseph Haule, Profesa Jay amesema kutokusomana tabia kwa muda mrefu ni moja ya sababu inayochangia ndoa nyingi kuvunjika baada ya muda mfupi.

Profesa Jay alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumzia Siku ya Wapendanao ambayo inaadhimishwa Februari 14 na mwaka huu itakuwa Jumapili ijayo.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Profesa Jay alijitolea mfano yeye kwamba alifunga ndoa na mke wake, Grace Haule mwaka 17 baada ya muda mrefu wa kuwa katika mahusiano ya kawaida.

“Ni kipindi kirefu kilichokuwa na maana kubwa ya kusomana kwenye tabia, haiba na mambo mengine ambayo kwa siku hizi yamekuwa kikwazo kwa wengi kwakuwa wanafunga ndoa bila kujuana vizuri,” alisema.

Profesa Jay kwa sasa anayetamba katika kibao cha Mzazi alichoshirikishwa na Bonaventure Kabogo au Stamina alitoa wito kwa wapendanao kama wanahitaji kuingia kwenye maisha ya ndoa ni vyema kufanya tathimini ya kusomana kabla ya kufanya maamuzi ya kuingia kwenye hatua hiyo kubwa.

Chanzo: habarileo.co.tz