Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Profesa Jay atamani kuonana na Rais Samia

Profesa Jay Jizo Profesa Jay atamani kuonana na Rais Samia

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa zamani wa Mikumi na Msanii Staa Joseph Haule maarufu Prof. Jay amesema angependa kuonana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili ampe maua yake uso kwa uso kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwake uliowezesha kutibiwa Tanzania na India .

Akiongea kwenye Power Breakfast ya CloudsFM leo November 06,2023, Prof. Jay amesema “Nipo vizuri namshukuru sana Mungu kila siku nazidi kuimariki, namshukuru sana Rais wa Tanzania alinipigania kunilipia matibabu yangu hapa Tanzania na India pia”

“Nilienda India katikati hapa kwahiyo namshukuru sana Mh. Rais ningependa sana siku moja nipate nafasi ya kuonana nae ili nimshukuru uso kwa macho kwasababu kitendo alichokifanya ni kama Mama kwa Mtoto nina kila sababu ya kushukuru na kumpa maua yake”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live