Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prof Jay aingia studio baada ya kupona

PROF JAY STUDIO Prof Jay aingia studio baada ya kupona

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msaani nguli wa Hip-Hop Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ameonekana akiwa studio akirekodi wimbo ikiwa ni baada ya mwaka mmoja tangu atoe nyimbo ya Hands Up aliyomshirikisha G-Nako.

Jay ameonekana akiwa studio kwa Binladen ambapo aliandika ujumbe kwenye mitandao yake kijamii uliosomeka; “Asante Mungu, back to the business again, studio session with my young brother Binladen,”

Ikumbukwe takribani miezi 16 imepita tangu alipoanza kupigania maisha yake kitandani, Januari 2022, alijitokeza hadharani mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu baada ya kupona na kuchapisha jumbe kwenye mitandao yake akiwashukuru madaktari, Mungu na viongozi kwa maombi na misaada yao kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live