Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prodyuza Abbah afunguka sakata le Diamond kudai kutaka kumsaini Marioo

Abbah Process.jpeg Abbah Process

Wed, 4 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtayarishaji wa muziki hapa nchini, @abbah_process amemjia juu msanii Baba Levo baada ya chapisho lake katika mtandao wa instagram kuhusiana na Marioo kumfuata mara kadhaa nyota Diamond na kumsihi amsaini kwenye lebo yake ya WCB.

Kupitia chapisho hilo lipo katika ukurasa wa Baba Levo, Abbah ameacha ujumbe unaomtaka msanii huyo aache kukurupuka na kutetea upande moja wakati ukweli wote anaujua.

“Baba Levo sio kila kitu ni cha kukurupuka na kukipa nafasi kwa ukubwa wakati wewe unajua ukweli wote wa jambo hili...

Sasa najiuliza unataka kutengeneza nini kati yao” Abbah.

Hili limekuja baada ya Marioo kukanusha taarifa kuwa amekuwa akimfuata Diamond mara kadhaa na kuomba kusainiwa kwenye lebo ya WCB.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live