Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Priyanka ampongeza mumewe kwa malezi ya binti yao

Pri Yankaaaa Priyanka ampongeza mumewe kwa malezi ya binti yao

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji kutoka nchini India, Priyanka Chopra amempa pongezi mumewe Nick Jonas na watu wengine walioshiriki kumlea binti yake Malti kwa wakati alipiokuwa katika kazi yake ya sanaa.

Tovuti ya The People News imeeleza kuwa mwigizaji huyo weekend hii ame-share picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na familia yake baada ya kutoka kuigiza nchini Australia na kutoa pongezi kwa watu waliyo mlea binti yake akiwemo mumewe.

“Hakuna kitu kama familia, mume wangu na marafiki kukufanya upate nguvu mpya kwa kunitunzia malaika wangu” ameandika.

Mwigizaji huyo, mwenye umri wa miaka 41, siku chache zilizopita alionekana Australia ana ‘rekodi’ filamu ya ‘The Bluff’ ambayo iko katika hatua za mwisho kutoka, kulingana na maelezo yake baada ya ku-share picha mtandaoni.

Ikumbukwe kuwa Chopra na Jonas walifunga ndoa ya Kikristo mwaka 2018 katika Jumba la Umaid Bhawan nchini humo na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live