Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Prince Harry na mkewe Meghan waanza ziara Nigeria

Meghan Harry 60332 Prince Harry na mkewe Meghan waanza ziara Nigeria

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamfalme Harry na mke wake Meghan wamewasili nchini Nigeria kwa ziara ya siku tatu.

Hii ni safari yao ya kwanza nchini humo kama wanandoa, na inakuja baada ya Mwanamfalme Harry kuhitimisha ziara fupi ya London.

Prince Harry na Meghan walialikwa na mkuu wa ulinzi wa Nigeria, Jenerali Christopher Musa, na watakutana na wafanyikazi waliojeruhiwa.

Ziara yao ni sehemu ya mfululizo wa matukio yanayohusishwa na Michezo ya Invictus, tukio la michezo kwa wanaume na wanawake wa kijeshi waliojeruhiwa iliyoanzishwa na Prince Harry ambayo inaadhimisha mwaka wake wa 10 mwaka huu.

Wanandoa hao waliwasili mjini Abuja Ijumaa asubuhi, na kuanza ziara yao kwa kutembelea Lightway Academy, shule ya msingi na sekondari katika mji mkuu.

Walipokelewa na wacheza ngoma za asili na kukutana na baadhi ya watoto wa shule ya msingi.

Wanandoa hao kisha waliendelea na uzinduzi wa mkutano wa kilele wa afya ya akili wa siku mbili, baada ya hapo mkuu huyo ataelekea katika kituo cha ukarabati wa kijeshi huko Kaduna.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live