Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Prince Harry na Meghan wafuatiliwa na waandishi

Nyeww Prince Harry na Meghan wafuatiliwa na waandishi

Thu, 18 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tukio hilo lilitokea baada ya familia hiyo ilipohudhuria sherehe za tuzo zilizofanyika mjini New York zilizoandaliwa na Ms.Foundation for Women ambapo Meghan alipatiwa tuzo kwa kazi zake anazofanya

Prince Harry wa Uingereza akiwa na mke wake Meghan pamoja na mama wa Meghan walijikuta wakifuatiliwa na gari lililowabeba waandishi wanaochukua picha, msemaji wa Harry amesema leo Jumatano.

Tukio hilo lilitokea baada ya familia hiyo ilipohudhuria sherehe za tuzo zilizofanyika mjini New York zilizoandaliwa na Ms.Foundation for Women ambapo Meghan alipatiwa tuzo kwa kazi zake anazofanya.

Picha ambazo zimeonekana kwenye mitandao ya kijamii zinawaonyesha Harry, Meghan na mama wa Meghan, Doria Ragland wakiwa ndani ya Taxi. “Jumanne usiku The Duke and Duchess of Sussex na Miss Ragland walijikuta wakifuatiliwa na gari lililokuwa na wapigapicha”, msemaji alisema katika taarifa hiyo.

Harry na Meghan walijiondoa kutoka jukumu la kazi za kifalme mwaka 2020 na walihamia Marekani kwa kile walichokieleza usumbufu wa hali ya juu wa vyombo vya habari.

Harry kwa muda mrefu amekuwa akizungumza kuhusu hasira zake za kufuatiliwa na vyombo vya habari ambapo anavilaumu kupelekea kifo cha mama yake Princess Diana ambaye alifariki wakati gari lake lilipopata ajali likiwa linawakimbia waandishi wa habari waliokuwa wakimfuatilia mjini Paris, Ufaransa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live