Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pretty Kind ageukia muziki wa Injili

Pretty Kind 000 Pretty Kind ageukia muziki wa Injili

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji wa Gospel na muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Suzan Michael maarufu kama Pretty Kind amesema anawakaribisha mashabiki wake wote kusikiliza wimbo wake mpya wa Gospo unaokwenda kwa jina la Alpha na Omega.

Pretty Kind amesema; “Bwana Yesu asifiwe, ninaitwa Pretty Kind, mpendwa ninakukaribisha kutazama wimbo wangu mpya wa #Alpha na Omega.

“Ninakuomba pia sambaza kwa wengine wimbo huu ufanyike kuwa baraka kwao kwa jina la Yesu. Usisahau ku-Share, ku-Like, ku-Comment na ku-Subscribe chaneli yangu. Mungu Akubariki Sana!”

Ikumbukwe kuwa, msanii huyo aliwahi kufanya muziki wa Bongo Fleva, bongo movie, modeling. Msanii huyo pia alishawahi kutajwa kwenye skendo ya kubakwa na kudanga nchini India miaka ya nyuma kabla hajarejea nchini na kuokoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live