Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Pomboo anavyoakisi ubinadamu kwa walimwengu

Mbele Pombo Pomboo anavyoakisi ubinadamu kwa walimwengu

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sina shaka utakuwa umeshawahi kulisikia jina la Pomboo, huyu ni Mnyama ambaye ana sifa za kustaajabisha na wengi wenu mnamfahamu kwa jina la lugha ya kigeni yaani Dolphin.

Pomboo ni jamii ya Samaki lakini anazaa na kunyonyesha, lakini anapozaa huanza kumtoa mtoto mkia na si kichwa. Sifa yake kubwa ni kuwa na kasi kubwa sana majini na hupendelea kucheza muda mwingi na mdomoni ana meno yapatayo 100 wakiwa na namna yao ya kuwasiliana kwa lugha tena kwa sauti, pia ni kiumbe mpole na mwenye akili myingi.

Urafiki na Binadamu.

Ni ngumu sana kwa viumbe hawa kuwa na urafiki baina yao wanyama ya makundi tofauti, walioliweza hili ni mamba na kiboko tuu, lakini hapa anajitokeza Pomboo, kiukweli huwezi kufa maji kama Samaki huyu anakuona unatapatapa ni muokoaji kabisa, lakini pia huwezi kupata madhara ya kushambuliwa na Samaki wakali kama papa, halafu Pomboo akakuacha kwani atakulinda kwa hali na mali.

Inapotokea umedumbukia majini na akakuona haraka sana hukufikia, kisha atakukumbatia na kwa spidi kubwa atakuwa anakupeleka nchi kavu, atakapofika jirani atakachokifanya ni kukurusha nchi kavu na msaada wake unakuwa unaishia hapo, ukitua kwenye jiwe, mwamba, michongoma, mtini shauri yako yeye kazi yake ashamaliza, pole utapewaga na wasamaria.

Upo ushahidi pia kuonesha ya kwamba Pomboo kuwahi kuwasaidia watu katika mazira mbambali kama hayo, kuna hadithi kuwa siku moja kuna Meli ilipita ukanda wa Samaki hao, kisha wakaanza kuifuata, nahodha mmoja alipotambua Pomboo wanafuatilia chombo chake alimua kusimama, ili aweze kuwatizama vyema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live