Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yawatoa kinguvu mashabiki shoo ya Mzee

Show+pic Polisi yawatoa kinguvu mashabiki shoo ya Mzee

Sat, 8 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

LICHA ya shoo 'Narudi Mjini' kuisha saa 9:00 usiku, bado mashabiki wa Mzee Yusuf walionyesha kuwa na hamu ya kuendelea nayo na kulazimisha askari polisi kutumia nguvu kuwatoa ukumbini hapo.

Tukio hilo lilitokea baada ya shoop kumalizika, lakini mashabiki wakaendelea kubaki ndani ya ukumbini kulikofanyikia shoo hiyo wakipiga vilaji na wengine wakipiga stori, licha ya uongozi wa ukumbi huo kuwataka waondoke.

Mashabiki hao ni kama hawakuwaelewa mabosi wa ukumbi huo uliopo Mbagala kwani walionekana kugoma kabisa kutoka mpaka pale askari polisi walipoingilia kati na kuwaondoa.

"Muda wa shoo umeisha nendeni majumbani kwenu," alisikia polisi mmoja akiwaondoa watu katika eneo hilo.

Mmoja wa mashabiki aliyejitambulisha kwa jina la Sabrina Khaleed, amesema alibaki eneo hilo kwa lengo la kutaka kumshika hata mkono Mzee Yusuf kwani walimmisi kumuona muda mrefu.

Naye Jamal Kim, amesema walipenda shoo hiyo ingekesha mpaka asubuhi, kwani Mzee Yusuf ana vitu vingi vya kuwaimbia, hivyo kukaa mpaka asubuhi kusingemuathiri kitu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz