Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yatinga zahanati alikopelekwa Pascal Casian

42498 Pic+pascal Polisi yatinga zahanati alikopelekwa Pascal Casian

Tue, 19 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Polisi imetinga zahanati ya Kinga Mawimbi  iliyopo Mburahati jijini Dar es Salaam ambayo msanii Flora Mbasha, mumewe Daudi Kusekwa na mke wa Pascal Casian, Getruda Mashaka walipodai walimpeleka kumchoma sindano ya kutuliza maumivu.

Hatua hiyo inakuja baada ya leo Februari, 18, 2019  kuzuka taharuki ya Casian kutafutwa zaidi ya saa tatu alipoenda kuchukuliwa nyumbani kwake kwa ajili ya kupelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu.

Tukio hilo limesababisha Flora Mbasha, mume wake Mpoto, mke wa Pascal Casian, kuhojiwa kwa saa kadhaaa na Polisi kwa madai ya kumtorosha Casian na kumpeleka kusikojulikana.

Baada ya mahojino, walilazimika kuondoka na baadhi ya maofisa Polisi kwenda kwenye zahanati ambayo wanadai ndiyo walimpeleka  Casian  alipokuwa anatafutwa.

Leo, Casian alikuwa na ratiba ya kupelekwa hospitali ya Muhimbili baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuamua kumsaidia.

Casian ambaye alipata ajali Oktoba mwaka Jana Mkoani Singida, ilisababisha kupasuka kwa kibofu cha mkojo  . Akizungunza na Mwananchi baada ya mahojiano hayo, msanii Mpoto ambaye alikuwa akiratibu safari hiyo ya Muhimbili ya Casian, amesema kulitokea sintofahamu baada ya kwenda nyumbani kwa Casian kumchukua na kutomkuta.

Mpoto amesema walipokuwa wakipiga simu yake pamoja na ya mkewe wote wakawa hawapokoi.

Hivyo walijaribu kuwahoji majirani wanaokaa na Casian na mwenye nyumba wake ambaye aliwaeleza Kuwa amechukuliwa na marafiki zake  asubuhi na walimtaja Flora Mbasha na mumewe.

Baada ya kupata taarifa hizo, walimpigia simu Flora mara kadhaa bila kupata ushirikiano  huku akiwajibu mara kadhaa kuwa yupo busy, mara atawapigia baadaye na hata walipomuuliza kama yupo na mgonjwa aliwakatalia.

Baada yakupita saa mbili, Mpoto amesema Flora aliwapigia simu na kuwataarifu kwamba yupo njiani anaelekea Muhimbili hivyo wakutane huko.

Walipofika na mgonjwa Muhimbili na kuhojiwa na madaktari walikuwa wapi, aliwajibu kuwa  walienda kumchoma  sindano  ambayo hata hivyo walijikanganya hospitali waliyompeleka.

"Awali walituambia wamempeleka TMJ tukapiga simu huko tukiwa na Kamanda Mambosasa ambao walimjibu Kuwa hawajapokea mgonjwa wa aina hiyo kwa Leo.

"Ni kitokana na sintofahamu hiyo ndio ikaamuriwa wote tuje tuhojiwe Polisi, maana huwezi kujua sindano aliyochomwa isije ikaleta madhara baadaye halafu nia ya Mkuu wa Mkoa kumsaidia matibabu msanii mwenzetu ikabadilika,” amesema Mpoto.

Kwa upande wake mke wa Casian amesema walifikia hatua ya kumpeleka mgonjwa hospitali baada ya kuzidiwa. Amesema hali hiyo wameshaizoea na hospitali waliyoenda ambayo hakuwa tayari kuitaja jina, huwa wakienda hali inapobadilika.

Akizungumzia uhusiano wao na kina Flora, amesema ni watu wao wa karibu na wamekuwa wakiwasaidia mara kwa mara tangu  Casian aanze kuugua.



Chanzo: mwananchi.co.tz