Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yakamata Madawa Location ya "The Equalizer 3"

Denzel Washington Location Polisi yakamata Madawa Location ya "The Equalizer 3"

Sat, 5 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Italia limekamata Gramu 120 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine kwenye location ya utengenezaji wa filamu ya “The Equalizer 3” ya muigizaji Denzel Washington.

Hii imekuja kufuatia Kifo cha Mkuu wa idara ya Chakula kwenye Production ya filamu hiyo ambaye ameripotiwa kufariki kwa kuzidisha matumizi ya dawa hizo.

Baada ya polisi kufika kukagua mwili wa marehemu uliokuwa hotelini, walikuta vifurushi kadhaa vya Cocaine kwenye mfuko wa nguo ya marehemu hivyo kupelekea kuwapa polisi hisia kuwa kutakuwa na dawa za kulevya kwenye set ya filamu ya The Equalizer 3.

Tovuti ya TMZ inaripoti, wapishi kadhaa wametiwa mbaroni kufuatia tukio hilo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live