Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watoa ripoti ajali ya Michael B. Jordan

Michael B Jordan Polisi watoa ripoti ajali ya Michael B. Jordan

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia ajali ya gari aliyopata muigizaji Michael B. Jordan, weekend iliyopita sasa polisi wametoa ripoti kuhusiana na maendeleo ya muigizaji huyo na kueleza kuwa yupo salama na hajaumia sehemu yoyote.

Huku chanzo cha ajili hiyo kikiripotiwa kuwa gari ya Jordan iligonga gari nyingine iliyokuwa kimeegeshwa kando ya barabara, pia jeshi hilo la polisi limethibitisha kuwa muigizaji huyo hadi ajali inatokea hakuwa ametumia kilevi chochote.

Michael B Jordan alipata ajali ya gari, usiku wa Jumamosi Disemba 2, akiwa na gari aina ya Ferrari, ambapo ajali hiyo ilitokea nje ya Studio ya Sunset Gower mida ya saa 11 Alfajiri.

Jordan ameonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘Creed’, ‘Black Panther’, ‘Just Mercy’, ‘A Journal for Jordan’ na nyinginezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live