Mwigizaji nchini Marekani, Julia Fox anaendelea kutumia vizuri umaarufu mkubwa alioupata baada ya kuwa kwenye mahusiano na rapa maarufu Kanye West ‘Ye’.
Julia ameonekana akiianika kwa mapaparazi pochi yake mpya ya BIRKIN yenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 100 aliyozawadiwa na Kanye West kwenye birthday yake.
Kutokana na umaarufu huo hivi karibuni Julia alikuwa Paris Ufaransa kwa ajili ya kupiga picha za karida la Vogue.
Kwenye interview na New York Times, Julia aliongelea pochi hiyo akisema; “Kumiliki pochi ya Birkin na wewe sio tajiri inanipa wasi wasi kila wakati, mara kwa mara naitazama kama bado ipo na haijapotea tuu, ni stress kweli kuwa na hii pochi ya thamani".