Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pique hatihati kutolewa kwenye kikosini Barcelona

Pique Na Shakira Gfj.jpeg Pique hatihati kutolewa kwenye kikosini Barcelona

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez ana mpango wa kumuondoa beki mkongwe wa Barcelona na timu ya taifa ya hispania Gerald Pique katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, sababu kubwa ikiwa ni kuhofia kuzorota kwa ufanisi wa mchezaji huyo kutokana na kesi za kimahusiano dhidi yake na mpenzi wake wa zamani Shakira.

Xavi anahofia changamoto hizi anazopitia mkongwe huyo zinaweza zikadhoofisha ufanisi wake uwanjani hivyo anafikiria kumtoa katika mpango yake ya kikosi cha kwanza kwa faida ya timu hiyo. Hadi sasa Pique hajaanza katika mchezo wowote kati ya michezo ya ligi ambayo Barcelona wamecheza katika ligi kuu Uhispania msimu huu.

Pique ameonekana kurejea taratibu katika hali yake ya kawaida baada ya kuvunjika kwa mahusiano yake yaliyodumu kwa takribani miaka 12 na mwanadada mrembo Shakira ambaye pia ni mwanamuziki aliyevuma na vibao kadhaa kama wakawaka. Tangu kuachana kwao wawili hao wamefikishana mahakamani mara kadhaa katika kesi zilizohusu kudai mamlaka ya kuishi na watoto pamoja na mgawanyo wa mali.

Ingawa mchezaji huyo tayari ameonekana kuwa katika mahusiano mapya na mwanadada Clara Chia Marti ambapo kwa pamoja wameonekana wakihudhuria sherehe ya harusi lakini bado anaonekana kutorejea katika hali yake ya kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live