Katika mahojiano mapya na CNN, mwanasoka wa zamani wa #Barcelona #Pique amshutumu ex wake na mwimbaji wa pop wa Colombia, Shakira kwa kupotosha ukweli kuhusu kutengana kwao.
Shakira, 47, alitangaza kuachana na nyota huyo wa zamani wa Barcelona mnamo Juni 2022 huku kukiwa na uvumi kwamba alikuwa na msaliti wakiwa kwenye ndoa miaka 11 na watoto wawili pamoja.
Pique, 37, kwa sasa anachumbiana na Clara Chia Marti mwenye umri wa miaka 25, na pia amesisitiza kuwa ‘anafurahia sana penzi jipya ’ hata kama Shakira amekuwa akimshambulia mara kadhaa yeye na mrembo wake mpya.
Pique aliiambia CNN:
“Mwishowe, ukweli au kinachotokea hakielezwi kwa jinsi kilivyokuwa. Siwezi kudhibiti hili.
“Kitu kizuri zaidi ni kwamba mwishowe nimezungukwa na wapendwa wangu, familia yangu, marafiki zangu, watu wanaokujua sana. Wanajua ulivyo na unafanya nini, na hiyo inanipa amani sana.
Pique na Shakira walipata watoto wawili pamoja, Milan, 11, na Sasha, 9. Mnamo 2022, gazeti la Uhispania ‘El Periodico’ liliripoti kwamba wanandoa hao walikuwa wakiishi kando kwa wiki chache baada ya Pique kufukuzwa nyumbani na mwimbaji huyo wa pop.