Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pili: Nandy kaolewa wadangaji wamebaki

Pili Kitimtim Pili Kitimtim

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gladness Kifaluka almaarufu Pili Kitimtim; ni staa wa kike wa vichekesho nchini Tanzania kupitia kipindi chake cha Kitimtim ambaye anasema kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Nandy tayari ameolewa, lakini wadangaji wamebaki.

Pili ambaye ni shoga’ke Nandy anasema kuwa, amefurahi mno kwa Nandy kuolewa (ameolewa na rapa Nenga), lakini kamwe hawezi kuacha kusema ukweli kuwa wadangaji wamebakia, wanahangaika akiwemo na yeye.

“Ukweli ni huu hapa, tumpongeze tu Nandy maana mwenzetu ameshaolewa kazi ipo kwetu sisi wadangaji sasa hivyo namuomba Mungu sana na sisi atusaidie siku zote tupate wenza wetu,” anasema Pili ambaye naye ni mjamzito ambaye ujauzito wake na Nandy anasema wanapishana siku moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live