Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pierre Konki Liquid ambaye wengi hawamfahamu

46539 Pic+piere

Wed, 13 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii.  Ni utambulisho wa mwanamume aliyeishika mitandao ya kijamii wakati huu.

Huyu ni Peter Mollel aliyejizolea umaarufu baada ya video iliyomuonyesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka jana.

Leo Machi 13, 2019 ametembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha, umaarufu na mipango yake ya baadaye.

Pamoja na wengi kumfahamu kwa video hizo zinazomuonyesha akiwa kwenye vilabu vya usiku na baa, Pierre anasema yeye si mlevi kama wengi wanavyomtambua.

“Kuna mtu aliandika katika mitandao ya kijamii akisema mimi ni mlevi wa taifa, hilo halina ukweli wowote kwa kuwa nina shughuli zangu na huwa nakunywa baada ya mambo mengine, angeniita mnywaji angepatia,” amesema Pierre huku akitabasamu.

 “Mimi kama hamjui nina ofisi ya kuuza samani pale Keko na sofa moja nauza kuanzia Sh3 milioni, meza Sh1.2  milioni . Umaarufu pia umeniongezea chanzo kingine cha mapato. Katika shoo moja nalipwa hadi Sh3 milioni kwa usiku mmoja,” amesema Pierre.

Alipoulizwa kuhusu familia, Pierre mwenye umri wa miaka 42 amesema hajaoa na hana mtoto  na kueleza kwamba katika suala la ndoa hataki kukurupuka na kuja kujutia baadaye.

Wakati kwa upande wa ratiba yake ya kila siku, amesema huwa mara nyingi analala saa tisa usiku na kuamka saa nne asubuhi na jambo la kwanza analofanya ni kusali kwani anaamini Mungu ndio kila kitu pamoja na kwamba kwake starehe ni kila siku.



Chanzo: mwananchi.co.tz