Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Picha iliyozua mijadala ndoa ya Mrema na Doreen

Bibi Harusi Anachatii.jpeg Picha iliyozua mijadala ndoa ya Mrema na Doreen

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Lyatonga Mrema amefunga ndoa na Mkewe Doreen Mrema muda huu katika Parokia ya Uwomboni, Kiraracha Mkoani Kilimanjaro. Mwanasisa huyo mkongwe amefunga ndoa tena baada kumpoteza mke wake Bi Rose Mrema aliyefariki Septemba, 2022.

Miongoni mwa matukio yaliyoibua hisia tofauti ni baada ya picha yao ambapo Bi. Doreen ameonekana kuchati ama kusoma meseji, huku Mzee Mrema akiwa pembeni yake wakati ibada ya misa ya ndoa yao ikiendelea kanisani jambo ambalo si la kawaida.

Licha ya hilo, baadhi ya maoni ya watu wamekuwa wakisema mwanamama huyo amekwenda kula pesa za mzee Mrema jambo ambalo Doreen amelikanusha na kusema ana pesa zake za kutosha.

“Mimi si mwanamke wa kupewa, nimesimama mwenyewe na hata mali ninazo. Nilianza kujitafutia mimi, siendi kwake (Augustino Mrema) kutafuta mali. Lakini nikimlea vizuri akanipa mali si vibaya kwani ni mke wake,” Doreen mke wa Augustino Mrema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live