Meneja wa WCB Wasafi na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Babu Tale amemtaja Chibuzor Nelson Azubuike ‘Phyno’ kama Rapa wake bora ukanda wa Afrika Magharibi.
Utakumbuka Phyno kutokea nchini Nigeria, amewahi kushirikishwa na Staa wa Bongofleva kutoka Next Level Music (NLM), Rayvanny katika wimbo wake, Slow.
“Huyu ndiye mwanamziki pekee wa Hip Hop ninayemkubali West Africa” ameandika Baba Tale katika ukurasa wake wa Instagram.
Phyno alizaliwa Oktoba 1986 na kukulia katika Jimbo la Enugu, Nigeria, alianza kazi yake ya muziki kama mtayarishaji mwaka 2003, na anasifika kwa kurap katika lugha ya Igbo, huku akifanya kazi na wasanii kama vile Olamide, Wizkid, Davido, Timaya, Flavour, Ruggedman, Bracket, J. Martins na Mr Raw.