Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Petit Man azungumzia kudaiwa, utapeli

9833 Petiman+pic TZWeb

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shemeji wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Hamad Manungwa maarufu kwa jina la ‘Petit Man’ amefungukia ishu ya kudaiwa kuwa na madeni ikiwemo tuhuma za utapeli kwa baadhi ya watu.

Petit Man ambaye pia ni meneja wa wanamuziki mbalimbali Bongo, amefungukia ishu hiyo baada ya hivi karibuni katika mtandao wa Instagram kusambaa habari ya kuwa ana madeni mengi kwa watu na anaishi kwa utapeli.

Mwananchi lilizungumza na Petit na kusema kuwa, ukweli wa habari hiyo anaujua yeye hivyo hawezi kubishana na watu katika mitandao ya kijamii, kwani hata kama anadaiwa yeye si wa kwanza kudaiwa.

“Unajua mimi sibishani hata siku moja na watu wa mitandaoni kwa sababu najua wazi kuwa sio tapeli na wala sina madeni kama wanavyosema huko mitandaoni, na pia hata kama nadaiwa mimi sitakuwa wa kwanza kudaiwa hivyo sioni haja ya kuzungumzwa zungumzwa.

“Halafu mimi sijashtuka wala nini kuambiwa nina madeni kwani suala hili sijaanza kuambiwa leo, toka nimemuoa Esmah hilo ndilo neno lao, hivyo siwashangai kwani najua wanataka kunivunjia ndoa yangu tu,” anasema Petit Man.

Hata hivyo, Petit alikiri habari za kudaiwa analelewa na Esma na kusema kuwa asipolelewa na mke wake huyo atamlea nani?

“Hao watu wanaosema mimi nalelewa na Esmah wala hawasemi uongo ni kweli nalelewa, sasa nisipolelewa na mke wangu atanilea nani, tena mke wangu nampenda sana ananisababisha nionekane smati kila mara, kwa hilo namshukuru sana,” alisema Petit.

Chanzo: mwananchi.co.tz