Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Peter Msechu aonyesha mjengo wake

Msechu Nm Peter Msechu na familia yake

Sun, 13 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva na mshindi wa pili wa mashindano ya Bongo Star Seach wa mwaka 2009, Peter Msechu ameonesha nyumba yake mpya ya kuishi aliyoijenga Kibamba Jijini Dar es Salaam.

Msechu amesema amekua akidunduliza pesa kidogokidogo yeye na Mke wake kuanzia miaka 13 iliyopita (mwaka 2009) ambapo walikua wakihifadhi asilimia 50 ya kila pesa waliyokuwa wakiipata.

Msechu amesema kuwa pesa yake ya kwanza kuikata nusu kwa asilimia 50% ilikua ni shilingi milioni tano aliyoshinda kama Mshindi wa pili kwenye BONGO STAR SEARCH ikiwa ndio pesa yake kubwa kuishika kwa mara ya kwanza toka azaliwe huku Mshindi wa kwanza Paschal Kasian akishinda milioni 25.

"Nilipoamua kuwa na Familia na kuishi kama baba nilijiwekea malengo ya kuhakikisha naipa Furaha na Amani familia yangu kwa namna yoyote ile.

"Kuanzia mwaka 2009 mara tu baada ya kumalizika shindano la BSS mimi na mke wangu mama Lolo tulifanya maamuzi ambayo yalikuwa hayavumiliki wala kuwezekana kwani tulipitia magumu na yasiyoelezeka tulipokubaliana kuanza kusevu asilimia 50% ya kila pesa nitakayoingia kwa kazi yoyote ile ili tuweze kujenga.



"Haikuwa rahisi kwani kuna muda niligombana sana na mama Lolo kwani alitaka kujua kila hela ninayopata na alidai na kuhakikisha ile asilimia 50 tuliyokubaliana inatengwa na haitumiki kwa vyovyote vile.

"Tuligombana, tulikwazana tulifokeana ila leo hii mimi na mke wangu mama Lolo, watoto wetu watatu Lauren, Lian na Levin kwa furaha kubwa tunapenda kuwakaribisha nyumbani kwetu," amesema Msechu.

Nyumba hii ambayo alianza kuijenga mwaka 2017 ikiwa ni miaka 8 toka aanze kudunduliza kidogokidogo ina vyumba vinne vya kulala vyote vikiwa na choo na bafu ndani, sebule, dining na ofisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live