Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pesa ya kupewa na mume wangu siipi kipaumbele - Lulu

Lulu Majizzoges (29).jpeg Pesa ya kupewa na mume wangu siipi kipaumbele - Lulu

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu' wiki hii amezindua duka lake la pili la nguo, ambapo waandishi walipomuuliza kama mtaji wa duka lake la pili umetokana na faida ya duka la kwqnza au pesa amepewa na mume wake? amejibunkwa kueleza.

Lulu ambaye alipata umaarufu tangu akiwa mdogo, mbali na biashara zake binafsi lakini pia amekuwa ni balozi wa makampuni kadhaa.

Mrembo huyo anajenga nyumba yake ya kisasa Mbweni, Dar es salaam na alieleza kuwa ni moja ya matokeo ya juhudi zake katika kazi.

"Kusema ukweli wa Mungu kabisa nimefungua duka hili la pili sio kwamba labda kuna faida kubwa kwenye hii biashara, nafanya kwasababu ni kitu ambacho nakipenda.

"Hakuna hela ya mume wangu hapa ni pesa yangu mwenyewe ninayodunduliza kwenye mambo yangu mengine nimeamua kuiwekeza huku.

"Mume wangu ana uwezo wa kunifungulia duka kubwa zaidi ya hili, lakini mimi inanifundisha nini? Najifunza nini kama kila kitu nitakuwa mtu wa kufanyiwa, tupo kwenye maisha ambayo inabidi wewe mwenyewe usumbue akili yako," amesema Lulu ambaye ni mama wa watoto wawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live