Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pesa kubwa kuipata Konde Gang ilikuwa Mil. 4- Anjella

Pesa Kubwa Kuipata Konde Gang Ilikuwa Mil. 4  Anjella Pesa kubwa kuipata Konde Gang ilikuwa Mil. 4- Anjella

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: Radio Jambo

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Anjella amefunguka namna alivyokuwa akipokea Pesa kutokana na kazi zake huku akiweka wazi kuwa Mkataba wake na Lebo ya Muziki ya Kondegang ilikuwa anapokea asilimia 40 kwa mapato ya kazi zake.

Mbali na hivyo amefunguka kuwa Kipato kikubwa alichowahi kupokea kutokana na kazi zake ni Sh.Milioni 4 ambazo zililimbikizwa kwa muda wa miezi 3 au 4 ndio akapata kiasi hicho.

Licha ya hivyo #Anjella amefunguka kuwa sababu kubwa iliyofanya Lebo hiyo kuvunja mkataba nae ilikuwa ni kuchelewesha kuwasilisha kazi (Album) na kipindi hicho alikuwa anaumwa hivyo alishindwa kufanya hivyo.

Chanzo: Radio Jambo