Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paulina: Nitamzalia Dogo Janja mpaka achoke mwenyewe

Janjarooo A0009 Dogo na mpenzi wake

Sun, 19 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupata mtoto wa kiume anayeitwa ‘Ahyan’ mke wa msanii wa Hip Hop Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ anayeitwa Paulina Onna maarufu ‘Quenlinnatotoo’amepanga kuendelea kuzaa na mumewe watoto wengi zaidi.

Quenlinnatotoo’ amesema baada ya kugundua watoto wanakuja na Baraka na kufanya baadhi ya fursa za kimaisha kufunguka zaidi, itakuwa sababu ya kuendelea kupata watoto na mumewe.

Akizungumza nasi, Quenlinnatotoo amesema kwanza haoni shida kwenye malezi lakini kabla ya mtoto huyo tayari alikuwa na wengine anaowatambua kama watoto wake.

“Sina changamoto yoyote ile kwenye malezi ya mtoto nafurahia sana kulea, mimi hata kabla ya kuwa na mtoto tayari nina watoto ambao nawatambua kama watoto wangu kwahiyo hapo kwenye idadi ya watoto sina hesabu,”

“Napenda watoto nalea watoto wengi zaidi, ninao mpango wa kuongeza mtoto mwingine huko mbeleni na mume wangu Dogo Janja.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live