Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paula atumika kama fimbo kwa Kajala

Paula Apishana Na Mama Yake Paula atumika kama fimbo kwa Kajala

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juma Lokole; ni mtangazaji wa Wasafi ambaye kabla ya muigizaji Kajala Masanja au Mama Pau kumrudia msanii wa Bongo Fleva, Harmonize walikuwa marafiki, lakini sasa wamegeuka maadui.

Hata hivyo, habari mpya ni kwamba, Lokole amejikuta akishambuliwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudaiwa kumtumia binti wa Kajala, Paula Kajala au Pau kama fimbo ya kumchapia mama yake huyo kwa kitendo chake cha kumrudia Harmonize au Konde Boy.

Lokole anadaiwa kumtumia Paula kuvujisha siri za ndani za penzi la Harmonize na Kajala (Harmojala) huku akimtumia pia kuonesha ulimwengu kwamba hata mtoto wa Kajala hakubaliani na uamuzi wa mama yake wa kumrudia Harmonize.

Lokole anadaiwa kumjaza Paula sumu ili asikubali kuungana na mama yake kwa kile alichokifanya; ikumbukwe kwamba Lokole na Paula wanaitana Anko na wamekuwa marafiki wa muda mrefu.

Kabla ya Kajala kurudiana na Harmonize, Lokole ndiye alikuwa msemaji wa familia ya Kajala na Paula.

Sasa; Lokole aliposti video ya Paula akikata mauno huku akionesha cheni yake ya kiunoni na kuandika; “Hii ndiyo roho yangu…” Akimaanisha Paula ndiye roho yake.

Katika siku ya Kajala kuvishwa pete ya uchumba na Harmonize pale Serena Hotel jijini Dar, Paula alihudhuria, lakini saa chache mbelea alimkataa Harmonize kuwa baba yake wa kambo.

Paula ni mpenzi wa msanii Rayvanny wa Wasafi japo kuna uvumi kuwa wameshatengana.

Katika kupinga Harmonzie kuwa baba yake wa kambo, Paula alitumia ukurasa wake wa Instagram kubadilisha picha yake ya utambulisho na kuweka picha ya zamani akiwa mtoto; picha ya pamoja akiwa na mama’ke, Kajala na baba’ke wa kumzaa, P Funky Majani.

Kama bado haitoshi, Paula aliposti picha hiyo na kuifuatisha kwa maneno kwamba hiyo ndiyo familia yake halisi; yaani mama’ke Kajala na baba’ke Majani kuashiria kwamba katu hawezi kumtambua Harmonize kama baba wa kambo.

Paula aliandika; “Familia yangu, Kajala na Majani…” Kama Paula akimkubali Harmonize kama baba’ke, basi sasa atakuwa rasmi ni babamkwe wa msanii Rayvanny, japokuwa kuna tetesi kwamba Rayvanny na Paula hawapo tena pamoja kimapenzi.

Inafahamika pia kwamba, Harmonize na Rayvanny ni maadui kwani wana bifu kali mno hivyo kuna baadhi ya watu wa karibu wanasema huwenda Paula akatumika kumuangusha Harmonize kimuziki kwa kuvujisha siri za kambi kwa maadui wake kama Lokole.

Lokole amekuwa akitangaza waziwazi kwamba hana urafiki wowote na Harmonize na kundi zima la watu wa Konde Gang.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live